UMESIKIA HII KUTOKA KWA “NAY WA MITEGO”A.K. THE TRUE BOY

(News) NATISHIWA KUUWAWA KISA WIMBO WA SALAM ZAO

Hit maker wa Muziki gani na Salam Zao Nay Wamitego ameiambia MJ FM ARUSHA kuwa anapata vitisho vingi sana kupitia wimbo wake wa Salam zao.

Akiongea na Dj Haazu kwenye Kipindi cha DUNDO Nay amesema mara kwa mara amekuwa akitoa nyimbo zake anapokea vitisho vikalai sana kwa sababu ya style ya Muziki wake ambao anaufanya mziki ambao amesema sio Mziki wa Diss wala Uchokozi bali ni Ukweli anaoungea kwenye Ngoma zake kitu ambacho wengi wanakichukulia kama Diss au Uchokozi wa Kimaksudi.

Ney amesema kupitia wimbo wa Salam zao amepata Vitisho vingi sana vya kuuwawa hadi kufikia hatua ya kuingiwa na woga sasa kwani wengi wanamtishia kumuua na wengine wakimtishia kumpoteza kimziki.


0 comments: