HIZI NDIZO HATARI ZITOKANAZO NA UTOAJI MIMBA
Tuesday, October 15, 2013
Utokaji
mimba (Abortion) hutokea pale ambapo kiumbe kilicho chini ya wiki 22
kinapotoka kwa sababu moja ama zaidi au kinapotolewa kwa njia yoyote
ile.
Utokaji au utoaji wa mimba upo wa aina nyingi na husababishwa na vitu mbalimbali kama vile magonjwa, utumiaji wa sigara au pombe, madawa na wengine hawataki kuzaa, hivyo kutumia njia isiyoruhusiwa kisheria ya kutoa mimba.
Njia hizo za kutoa au kutoka mimba ni hizi zifuatazo:
Utokaji wa mimba usioepukika (Inevitable Abortion): Ni vyema kufahamu kwamba utokaji mimba wa namna hii hutokea ikiwa inatishia kutoka ingawa bado haijatoka (Threatened Abortion) au kwa kuwa mimba hiyo inakuwa haiepukiki kutoka.
Utokaji wa mimba ulio kamili (Complete Abortion): Utokaji wa mimba usio kamili (Incomplete Abortion), mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (Missed Abortion) na utokaji wa mimba unaojirudiarudia (Recurrent Abortion).
Utoaji mimba kinyume cha sheria (Illegal Abortion): Utoaji mimba kwa sababu za kiafya (Therapeutic Abortion) na utokaji mimba kwa hiari au kitendo cha mimba kutoka yenyewe (Spontaneous Abortion).
Hali hii hutokea mimba inapoharibika na kutoka bila kuwepo sababu zozote za kimatibabu zilizo wazi.
Kwa maneno mengine tunaweza kusema mimba huharibika na kujitokea bila kusababishwa na mtu wala kitu chochote.
Mimba isiyoepukika kutoka (Inevitable Abortion): Hutokea mapema wakati wa ujauzito pale damu inapotoka ukeni wakati njia ya shingo ya kizazi ikiwa imefunguka au kuwa wazi.
Hali huwa mbaya kwa sababu kiasi cha damu kinachotoka ni kingi na mgonjwa hujisikia maumivu makali sana ya tumbo.
Mimba inayotishia kutoka (Threatened Abortion): Ujauzito unapokuwa mchanga tatizo hili huweza kutokea. Hali hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haiambatani na maumivu yoyote ya tumbo lakini daktari anapompima mgonjwa hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga.
Utokaji wa mimba ulio kamili (Complete Abortion): Ni mbaya zaidi kwani mjamzito hutokwa na damu nyingi sehemu za siri na kujisikia maumivu makali ya tumbo pamoja na kutoka kwa kiumbe ikiambatana na kondo lake la nyuma.
Utokaji mimba usioepukika unaweza kusababisha utokaji mimba ulio kamili (Complete Abortion), au usio kamili (Incomplete Abortion).
Utokaji wa mimba usio kamili ni hatari kwa kuwa mgonjwa hutokwa na damu nyingi sehemu za siri na njia ya shingo ya kizazi hufunguka hivyo kutoka baadhi ya mabaki ya kiumbe (Products of Conception) ingawa mengine hubakia na kusababisha matatizo yapelekeayo kifo

0 comments: