TATHMINI YA MECHI YA WATANI WA JADI ILIYOMALIZIKA HIVI PUNDE

  NA SIMBA KUFANYA MAAJABU....!

Kila aliyeingia uwanjani alikaguliwa. Magari yote isipokuwa yale maalumu, na pikipiki zilizuiliwa kuingia ndani. Kutokana na kuhakiki hilo barabara inayotokea Keko kuelekea uwanjani eneo ya TCC imefungwa kwa kutumia malori mawili makubwa. (picha, maelezo Sufiani Mafoto blog).
Jumapili ya leo imewakutanisha watani wa jadi katika soka kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu za Simba na Yanga.

YANGA 3:3 SIMBA

Saleh "Jembe" kwenye blogu yake anaripiti kuwa dakika ya 15, Ngassa anaifungia Yanga bao baada ya kuiwahi krosi ya Kavumbagu na kuandika bao. Dakika ya 36, Kiiza anaifungia Yanga bao la pili baada ya beki Shamte kujichanganya mpira wa
kurusha wa Twite ulioguswa na Kavumbagu kwa kichwa. Dakika ya 45, Kiiza tena anaifungia Yanga bao la tatu baada ya Kavumbagu kugongeana vizuri na Niyonzima. Dk 53 Mwombeki anaipatia Simba bao moja baada ya pasi nzuri ya Tambwe. Dk 57, Owino anaifungia Smba bao la pili baada ya kuunganisha vizuri mpira wa kona wa Messi wakati mabeki wa Yanga wakimuangalia.

Shaffih Dauda kwenye blogu yake anasema, licha ya Yanga kuongoza, mashabiki watatu wa Yanga wamezimia na kupewa huduma ya kwanza. Kikosi cha timu ya Yanga kinachoanza ni: Barthez, Twite, Luhende, Cannavaro, Yondani, Chuji,  Niyonzima, Domayo, Kavumbagu, Ngassa, Kiiza.
Subs: Deogratia Munisi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva, Rajab Zahir, Jerson tegete, Nizar Khalifan

Wakati kikosi cha Simba kinachoanza ni: Dhaira, Cholo, Shamte, Kaze, Owino, Mkude, Singano, Humud, Mwombeki, Tambwe, Chanongo.
Subs: Abuu Hashim, Hassan Khatir, Issa Rashid, Zahoro Pazi, Amri Kiemba, Said Hamisi, William Lucian.

Awali, timu za vijana za Simba na Yanga, zilimaliza dakika 90 kwa kutoka suluhu ya kufungana bao 1-1 ambapo Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao na Simba wakasawazisha dakika tatu kabla ya kwenda mapumziko. Simba vijana wananolewa na kiungo wa zamani, Selemani Matola na Yanga inanolewa na kiungo wa zamani, Salvatory Edward.

0 comments: