URUGUAY, MARA YA 4 MFULULIZO, KWENDA KOMBE LA DUNIA KWA UANI?



Print PDF
Sunday, 13 October 2013 21:24
>>ARGENTINA, COLOMBIA ZIPO BRAZIL, CHILE, ECUADOR KUUNGANA NAO?
>>TIMU YA TANO KUCHEZA MCHUJO NA JORDAN!!
EDINSON_CAVANIJUMANNE Usiku, Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini, zinamaliza Mechi zao za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 na tayari Argentina na Colombia zimetinga huko Brazil huku Ecuador na Chile zikiwa na nafasi kubwa kunyakua nafasi mbili zilizobaki na kuiacha Uruguay ikihaha kupata nafasi kwa kupitia Mechi ya Mchujo.
Baada ya kuchapwa Bao 1-0 huko Quito na Ecuador hapo ijumaa, Uruguay wanaelekea kuwa watamaliza Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini katika Nafasi ya 5 na hivyo kukosa nafasi ya kwenda Brazil moja kwa moja na badala yake kupitia Mechi ya Mchujo, na hii itakuwa ni mara yao ya 4 mfululizo kucheza Fainali za Kombe la Dunia kupitia Mechi za Mchujo.
Kocha wa Uruguay Oscar Washington Tabarez amezungumza: “Mimi siko na wale wanaodhani kucheza Fainali za Kombe la Dunia kupitia Mechi ya Mchujo haistahili. Tulikwenda Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2010 kupitia Mechi za Mchujo na tulifanikiwa kumaliza Nafasi ya 4! Hatwendi kwa kupitia Mlango wa nyuma!”
+++++++++++++++++++++++++
MAREKANI YA KUSINI
ZIMEFUZU: Argentina, Colombia
MSIMAMO:

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Argentina
15
9
5
1
33
12
21
32
2
Colombia
15
8
3
4
25
12
13
27
3
Ecuador
15
7
4
4
19
14
5
25
4
Chile
15
8
1
6
27
24
3
25
5
Uruguay
15
6
4
5
22
23
-1
22
6
Venezuela
16
5
5
6
14
20
-6
20
7
Peru
15
4
2
9
16
25
-9
14
8
Paraguay
15
3
3
9
16
29
-13
12
9
Bolivia
15
2
5
8
16
29
-13
11
**FAHAMU: Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA, ambayo ni Jordan, kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZA MWISHO:
[Saa za Bongo]
Jumatano Oktoba 16
02:30 Paraguay v Colombia
02:30 Chile v Ecuador
02:30 Uruguay v Argentina
05:15 Peru v Bolivia
+++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Uruguay bado wana nafasi finyu ya kufuzu kuwa moja ya Nchi 4 zinazofuzu moja kwa moja ikiwa vitu viwili vitatokea kwenye Mechi za mwisho za Jumanne.
Kwanza, Uruguay ni lazima waifunge Argentina kwenye Mechi yao ambayo watacheza Nyumbani kwao na Timu ambayo tayari ipo Brazil na itacheza bila ya Supastaa Lionel Messi ambae ni Majeruhi.
Pili, ni lazima huko Mjini Santiago, Nchini Chile, apatikane Mshindi katika Mechi kati ya Wenyeji Chile na Ecuador na pia, ikiwa Ecuador atafungwa basi Magoli inabidi yabadilike kwa idadi ya tofauti ya Bao 6 na akifungwa Chile idadi hiyo ni Bao 4.
Hicho ni kitu kigumu hasa kwa vile tu Chile na Ecuador wanajua fika Sare kati yao inazibeba Timu zote mbili kwenda Brazil.

Kutoa maoni


0 comments: