SIKIA ALICHOKISEMA NAY WA MITEGO BAADA YA KUTISHIWA KIFO

Wednesday, 16 October 2013

HUU MZIKI UTANITOA ROHO SINA BEEF NA MTU ILA KUNA WATU WANATAKA HATA NIFE LEO"

Nay wa Mitego anahisi maisha yake yapo hatarini kwa sasa baada ya vitisho kutoka kwa watu mbalimbali kuendelea kumwandama.
Rapper huyo wa Salam Zao, ameshare taarifa hizo kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

“Huu muziki sasa utanitoa roho..!! sinaga ugomvi na mtu lakini kumbe kuna watu wanachuki serious na wanatamani atanife leo au wanitoe roho..!! Mi nafanya muziki vita yenu juu yangu namuachia mungu#966 mi nafanya kazi nzuri..! Hakuna wakunirudisha nyuma,, logeni niwindeni kwa vyovyote mtafeli 2. Mi siko wakawaida kiivyo itakula kwenu,” aliandika.

Baada ya kauli hiyo Bongo5 ilimtafuta Nay, ambaye alisema kuwa muziki ni sehemu ya maisha yake na wala hataogopa chochote wala kusita kufanya kile anachoona astahili kukifanya.


“Nimeshaona jinsi gani muziki unaniongezea maadui nashangaa hata watu ambao sina ugomvi nao wana chuki na mimi na wapo tayari kunifanya chochote,” aliongeza.

0 comments: