KUHUSU UFOO SARO:
Kama ambavyo umepata taarifa kuhusu kupigwa risasi kwa Mwandishi na
Mtangazaji wa ITV na Radio One Ufoo Saro, taarifa zinaendelea kueleza
kuwa mtu aliyempiga risasi amejulikana kwa jina la Antel Mushi. Mtu huyo
pia alimpiga risasi mama mzazi wa Ufoo Saro ambaye alifariki papo hapo,
na yeye mwenyewe kujiua mara baada ya kufanya unyama huo.
Hivi sasa, Ufoo Saro ameingizwa kwenye chumba cha upasuaji (theatre) kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.
Akizungumza katika hospitali ya taifa Muhimbili Mkuu wa upelelezi wa
Kanda maalum ya Dar-es-salaam Hemed Msangi amesema Ufoo amepata majeraha
tumboni na kwenye bega na kwamba upelelezi unaendelea kubaini chanzo
cha tukio.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald
Mengi amewaambia waandishi wa habari waliopo katika hospitali ya taifa
Muhimbili kuwa ana imani mtangazaji wa ITV na Radio One Ufoo Saro
atapata nafuu na kurejea katika hali yake ya kawaida wazidi kumuombea.
Dk. Mengi ameelezea kuridhishwa na huduma inayotolewa na madaktari
wanaomtibu Ufoo Saro ambaye kwa sasa yupo kitengo cha dharura cha
hospitali ya taifa Muhimbili alikomtembelea hivi punde.
Kama ambavyo umepata taarifa kuhusu kupigwa risasi kwa Mwandishi na Mtangazaji wa ITV na Radio One Ufoo Saro, taarifa zinaendelea kueleza kuwa mtu aliyempiga risasi amejulikana kwa jina la Antel Mushi. Mtu huyo pia alimpiga risasi mama mzazi wa Ufoo Saro ambaye alifariki papo hapo, na yeye mwenyewe kujiua mara baada ya kufanya unyama huo.
Hivi sasa, Ufoo Saro ameingizwa kwenye chumba cha upasuaji (theatre) kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.
Akizungumza katika hospitali ya taifa Muhimbili Mkuu wa upelelezi wa Kanda maalum ya Dar-es-salaam Hemed Msangi amesema Ufoo amepata majeraha tumboni na kwenye bega na kwamba upelelezi unaendelea kubaini chanzo cha tukio.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi amewaambia waandishi wa habari waliopo katika hospitali ya taifa Muhimbili kuwa ana imani mtangazaji wa ITV na Radio One Ufoo Saro atapata nafuu na kurejea katika hali yake ya kawaida wazidi kumuombea.
Dk. Mengi ameelezea kuridhishwa na huduma inayotolewa na madaktari wanaomtibu Ufoo Saro ambaye kwa sasa yupo kitengo cha dharura cha hospitali ya taifa Muhimbili alikomtembelea hivi punde.
0 comments: