MWANAMUIZIKI
aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam,
Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa
na utata mkubwa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo nchini China, rapa huyo
alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya
kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact,
Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.
“Tulijua
kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa)
tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na
nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu
aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.
Baada ya
kupata taarifa hizo Amani liliwasiliana na Kiongozi wa FM Academia,
Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot. Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa. “Haristot
alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya
kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli
hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi.
|
0 comments: