WATANZANIA JIJINI LUSAKA WAADHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA MICHEZO
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuna akiwakaribisha watanzania walioshiriki kwenye michezo mbalimbali wakati wakiadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu JK Nyerere kwenye Viwanja vya barclays jijini Lusaka Zambia
Kikosi cha Simba ya Lusaka kilichoshiriki mpambano mkali wa mpira wa Miguu na wahasimu wao Yanga wa Lusaka katika maadhimisho ya kifo cha baba wa Taifa Mwl Nyerere kwenye Viwanja vya barclays jijini Lusaka Zambia
Kikosi cha Yanga cha Lusaka kilichoshiriki mpambano mkali wa mpira wa Miguu na wahasimu wao Simba wa Lusaka katika maadhimisho ya kifo cha baba wa Taifa Mwl Nyerere kwenye Viwanja vya barclays jijini Lusaka Zambia
Hapa ni mpambano wa kuruka juu wa watanzania wa Kabila la Wamasai waishio Lusaka Zambia katika maadhimisho ya kifo cha baba wa Taifa Mwl JK Nyerere kwenye Viwanja vya Barclays
Juu na chini ni kina mama walioshiriki mpambano mkali wa kuvuta Kamba katika maadhimisho ya kifo cha baba wa Taifa Mwl Nyerere kwenye Viwanja vya Barclays jijini Lusaka Zambia
0 comments: