Tembo waua watu 14 Serengeti


Watu 14, ng’ombe 72, mbuzi 440, kondoo 60 wameuawa na mashamba 3042 yenye ekari zaidi ya 6287 yameharibiwa na wanyama wakali kama tembo kati ya mwaka 2009 mpaka sasa wilayani Serengeti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Goody Pamba alisema watu wanne walijeruhiwa katika kipindi hicho.
Pamba alisema pamoja na madhara hayo, kwa Mjibu wa sheria ya wanyama pori ya mwaka 2009, hakuna kifuta machozi kilichokwishatolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, hali ambayo inazidisha uhasama kati ya jamii na wahifadhi.


0 comments: