SIMANZI: MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU MAMA UFOO DAR!


Wakazi wa jiji la Dar Es Salaam wamejitokeza kuaga mwili wa mama mzazi wa mwandishi wa ITV Radio one Ufoo Saro marehemu Anastazia Saro katika kanisa la kiinjili la kilutheri Kibwegere Kibamba kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi kwa mazishi.
Kutokana na msiba huo,ITV ilianza kwa kufika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ili kumjulia hali mwandishi wa ITV Ufoo Saro aliyelazwa katika hospitali hiyo ambapo afisa uhusiano wa hospitali hiyo bwana Aminiel Aligaesha amesema anaendelea vizuri.
Baada ya afya ya Ufoo Saro inavyoendelea, ITV ilitia kambi katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo na kushuhudia mwili wa Anastazia Saro ukiondolewa na kupelekwa Kibamba nyumbani kwake ambapo umati mkubwa wa watu walipokea mwili huo kisha kuingizwa ndani huku vilio vikitawala.

Mwili ulifikishwa katika kanisa la KKKT Kibwegere Kibamba na kupokelewa na umati mkubwa wa watu waliofika ndani ya kanisa hilo,ambapo mchungaji wa kanisa hilo Magreth Chikolowa amesema kuwa kuna vifo vingine vinatokea lakini si kwa kusudi la Mungu huku msemaji wa familia akieleza historia fupi ya marehemu.

Mkurugenzi wa ITV Radio one Bi Joyce Mhaville kwa niaba ya mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr Reginald Mengi amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mama yake Ufoo na kwamba mbali na kuwepo hapo kwa ajili ya mwenyekiti wa makampuni ya IPP lakini ameagizwa na Ufoo Saro kumwakilisha katika kumuaga mama yake huku mwenyekiti wa kamati nzima wa msiba huo akitoa shukrani kwa mwenyekiti wa makampuni ya IPP kwa kufanikisha safari ya kusafirisha mwili huo kama anavyoeleza.

Ndugu jamaa na marafiki waliaga mwili huo kwa majonzi huku baadhi ya wafiwa wengine wakishindwa na kupewa msaada wa kushikwa huku vilio vikitawala ambapo marehemu Anastazia Saro ameacha mtoto mmoja Ufoo Saro na mjukuu mmoja Alvin ambapo anatarajia kuzikwa katika kijiji cha Shali Machame mkoani Kilimanjaro.

0 comments: