MSANII WA FILAMU NA MAIGIZO LULU ATUPA JIWE GIZANI

Monday, October 14, 2013

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewatolea uvivu watu ambao wana kasumba ya kuwahukumu wenzao kwa kujichora tatuu mpya ambayo imebeba ujumbe kwa watu ambao hakuwataja.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kupitia akaunti ya Instagram, mwishoni mwa wiki iliyopita, Lulu aliposti picha inayomuonesha akiwa amejichora tatuu iliyosomeka; Only God can judge me. Imeaminika kuwa maneno hayo ameandika kama ishara ya kuwapiga madongo watu wenye tabia ya kufuatilia maisha ya watu.
“Watu wanaongea na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine! Kwa upeo wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja, Mwenyezi Mungu…lakini cha kushangaza kuwa watu wako bize kuhukumu wenzao…ONLY GOD CAN JUDGE ME,” aliandika Lulu.

0 comments: