Mechi za kufuzu kombe la dunia barani Afrika (Part II).
Michezo ya kufuzu kwa kombe la dunia bara la Afrika imeendelea hii leo ambapo michezo miwili imepigwa huko Ethiopia na na nchini Tunisia .
Jijini Addis Abbaba timu ya taifa ya Ethiopia maarufu kama The Walya Antelopes walikuwa wenyeji wa Nigeria au The Super Eagles .
Katika mchezo huo Nigeria walishinda kwa matokeo ya 2-1 .
Mabao ya washindi yalifungwa na mshambuliaji anayecheza nchini Uturuki Emmanuel Emenike ambaye alifunga mabao yote mawili huku Ethiopia wakifunga kupitia kwa Mengistu Asseffa .
Katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Olimpiki jijini Tunis Cameroon na Tunisia walitoka sare ya bila kufungana .
Michezo hiyo itaendelea siku ya jumanne ambapo Ghana watakuwa wenyeji wa Misri katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Baba Yara huko Accra .
0 comments: