MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ametoa onyo kali kwa watu wanaotumia jina la mwanaye huyo kuuza filamu zao.
Akichonga
na paparazi wetu, Mama Kanumba alisema hivi karibuni kuna filamu
imetoka kwa watoto wa baba Kanumba waliopo Shinyanga ambayo imewekwa
nembo ya kampuni ya mwanaye, Kanumba The Great Film hivyo haitambui.
“Jamani kampuni ya Kanumba haina tawi Shinyanga kama filamu hiyo
inayosambazwa huko bali hiyo imechezwa na watu ambao hawatambuliki
katika kampuni ya marehemu mwanangu,” alisema Mama Kanumba. |
0 comments: